Thursday, October 17, 2013
POLE POLE POLE POLE
Mwanamke mmoja wa Ilala jijini Dar es Salaam, Mwanahamisi Saidi amefariki dunia wakati akijiandaa kwenda kwa mumewe baada ya kufunga ndoa.
Tukio hilo limesababisha sherehe ya harusi kugeuka kuwa msiba.
Tukio hilo la kuhuzunisha lilitokea Jumapili iliyopita, muda ambao bibi harusi alitakiwa kuchukuliwa na mumewe Amani Hassan kwenda nyumbani kwake.
Mwanahamisi aliaga dunia akiwa katika Hospitali ya Amana iliyoko Wilaya ya Ilala, baada ya kuugua ghafla.
Akizungumza kwa majonzi, Hassan alisema kuwa alifunga ndoa kwa taratibu za Dini ya Kiislamu Ijumaa iliyopita katika msikiti ulioko Vingunguti jijini Dar es Salaam na kupanga kwenda kumchukua mkewe siku ya Jumapili.
“Baada ya kufunga ndoa niliwaahidi ndugu wa mke wangu kuwa nitakwenda kumchukua mke wangu Jumapili kwa sababu upande wangu ulikuwa umeandaa sherehe iliyoanza Jumamosi na Jumapili ndio tulipanga kumaliza kwa kumchukua mwali wetu,” alieleza kwa masikitiko Hassan.
Alisema alipigiwa simu na mdogo wa marehemu kuwa mkewe ameugua ghafla na hana nguvu na kwamb
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment