Friday, October 18, 2013
TOA USHAURI WAKO
Natafuta njia ya kuachana naye
SWALI
Swali langu kwa Mshauri ni kwamba, mimi ni msichana ambaye nina mpenzi wangu niliyempa moyo wangu wote kwa kumwamini kuwa atakuwa mume wa maisha yangu. Lakini siku za hivi karibuni amebadilika, mara nyingi nimefuma meseji za mapenzi kwenye simu yake na wakati mwingine nimemuona laivu. Naumiasanalakini nashindwa kumuacha kwa sababu nampenda, mshauri nisaidie njia ya kumwacha mwanaume huyu ataniua bure.
JIBU
Kitaalamu mwanzo wa mapenzi huwa ni rahisi kuliko mwisho wake. Hii inatokana na ukweli kwamba mapenzi ni sawa na ulevi ambao mtu akiuzoea ni vigumu kuuacha kwa mara moja, ndiyo maana tunaona watu wanateswa lakini wanashindwa kuamua kuachana na wapenzi wao kwa sababukamahizo zako. Sasa ili mtu afikie uamuzi wa kuachana na mtu aliyekuwa nayekamampenzi kwa miaka mingi lazima ajue kanuni, vinginevyo moyo hautakubali.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment